Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimekanusha taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwa chama hicho kimechukua fomu za kugombea ubunge katika uchaguzi wa marudio jimbo la Singida Mashariki.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya CHADEMA, Tumaini Makene amemtaka Mkurugenzi wa NEC Ndugu Ramadhan Kailima kutojifanya msemaji wa chama hicho kwa hatua ya sasa na kudai kuwa wanafuatilia kupata taarifa za kina kuhusu kauli yake hiyo ambayo ameitoa leo Disemba 19, 2017 wakati akihojiwa na kituo kimoja cha Radio.
"Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakijateua mgombea kuwania nafasi ya ubunge katika uchaguzi huo wa marudio, Jimbo la Singida Kaskazini. Mkurugenzi wa NEC, Ndugu Ramadhan Kailima atambue kuwa suala la kugombea nafasi ya ubunge kwa mchakato wa ndani ya CHADEMA linasimamiwa na Kamati Kuu ya Chama na hivyo hivyo yeye hana mamlaka wala hawezi kuwa msemaji wa suala hilo katika hatua ya sasa" alisema Tumaini Makene
Makene aliendelea kusema kuwa "Tunafuatilia kupata taarifa za kina kuhusu msingi wa kauli ya Mkurugenzi hiyo, kisha tutatoa taarifa kamili katika hatua ya baadae"
CHADEMA walitoa msimamo wao kuwa hawatashiriki katika uchaguzi mdogo wa marudio wa nafasi za ubunge kama Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) haitaahirisha na kusogeza mbele uchaguzi huo katika majimbo matatu mpaka pale wadau wa siasa watakapokaa na kufanya tathmini juu ya kile walicholalamikia kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani ambao umefanyika karibuni hakuwa huru na haki, na ulitawaliwa na uvunjwaji wa haki za binadamu.
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: