Migodi ya Acacia Buzwagi na Bulyanhulu inayochimba madini aina ya Dhahabu, wilayani Kahama, Mkoani Shinyanga imeanza kutekeleza mpango wake wa kufunga shughuli za uchimbaji madini inayojulikana kwa Jina la “No Harm 2020” kwa kuwapatia wafanyakazi wake semina ya fursa za ajira ili kuwaandaa na maisha baada ya kufungwa kwa migodi hiyo.
Katika mgodi wa dhahabu wa Acacia Buzwagi, wafanyakazi wa Migodi hiyo wanakutana katika tamasha la ajira ambapo zaidi ya Kampuni 40 zinazojishughulisha mambo ya migodi zimejitokeza hapa kuonesha fursa walizonazo huku idadi kubwa ya watanzania wakiwa wamepatiwa mafunzo na uzoefu kutokana na uwepo wa migodi hiyo.
Baadhi ya watumishi wanaotarajia kusitishiwa ajira zao baada ya kufungwa kwa migodi hiyo wanasema fursa hiyo ya ajira inawaandaa kukabiliana na maisha baada ya migodi kwa kujiajiri wenyewe.
Dkt. Chris Mauki ni Mkufunzi katika idara ya Saikolojia ya Chuo kikuu cha Dar es salaam anatumia nafasi hiyo kuwapa moyo wafanyakazi hao kwa kujiandaa na maisha baada ya kufungwa kwa migodi hiyo huku kampuni za zinazotangaza fursa zaajira zikivutiwa.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: