UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Hali hii ni ya kusikitisha kwasababu mifugo hiyo ingeweza kuokolewa kwa kutumia njia rahisi zinazoeleweka kama matibabu ya mara kwa mara kwa ajili ya kutokomeza minyoo hiyo kwa kutumia dawa za minyoo zinazofaa kufuatana na eneo la mfugaji.
Ni muhimu sana kulisha mifugo malisho yaliyo safi kwenye mahori safi ambapo ndama au wanyama wengine watashindwa kuyakanyaga na kuyachafua.
Kwa kuzingatia swala hili kila siku kutasadia kuzuia maambukizi ya minyoo kwa mifugo. Iwa po mifugo inatunzwa kwa kuchungwa, ni vyema kugawa eneo la kuchungia katika sehemu ndogondogo na kuichunga mifugo hiyo kwa mzunguko.
Wanyama wataruhusiwa kuingia kwa kujilisha katika sehemu moja tu ya eneo hilo kwa kipindi cha muda fulani na malisho yatakapopungua katika sehemu hiyo ndipo watakapohamishiwa katika sehemu inayofuata ya malisho katika eneo hilo.
Kwa kufanya hivyo utaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa mifugo yako kuambukizwa minyoo kwa urahisi kutokana na malisho kuwa safi kwa kiasi kikubwa.
Wanyama pia waletewe maji nyumbani kuliko kuwapeleka kunywa maji lamboni kutokana na sababu kuwan maeneo wanakopelekwa kunywa maji yanaweza kuwa na minyoo hasa ile kwenye maini au mayai yake na hivyo mifugo hiyo kuambukizwa.
Njia ya pekee na nzuri zaidi ya kutosha kupambana na minyoo ni kuwapa mifugo dawa za minyoo mara kwa mara. Baadhi ya dawa hizo hutolewa kwa njia ya sindano, nyingine zikiwa na uwezo wa kuangamiza minyoo ya aina nyingi na nyingine zikiwa ni maalumu kwa ajili ya aina fulani tu za minyoo.
Uzuiaji wa kupe na mbung’o
Wadudu wanyonyao damu wakiwa nje ya mwili wa mnyama ni wengi sana isipokuwa magonjwa mengi yanayosababisha vifo vya mifugo huenezwa na kupe pamoja na mbung’o.
Kuna njia mbalimbali za kuweza kupambana na hali hii, mojawapo ikiwa ni ufugaji wa ndani ambao hupunguza uwezekano wa kupe kuwafikia wanyama.
Kuogesha wanyama kwa kutumia dawa za kuzuia kupe mbazo gharama zake ni ndogo zaidi ukilinganisha na gharama za kutibu mnyama aliyeambukizwa magonjwa yanayotokana na kupe. Dawa hizo ni kama vile Bayticol, Supona, Backdip, Delnav na nyinginezo kulingana na ushauri wa wataalamu wa mifugo.
Muhimuintro_01
Ili kukinga wanyama kuambukizwa magonjwa mbalimbali ni muhimu kwa mfugaji kuzingatia yafuatayo;
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA HABARI ZAIDI"
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: