UNGANA NA
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete ambaye kesho anatarajia kumkabidhi Rais Dk John Magufuli nafasi ya juu kabisa ya Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, mapema leo Julai 22.2016 katika Makao Makuu ya Chama, Dodoma, wakati wa kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) amesema kuwa chama hicho kitaendelea kutawala Nchi kutokana na misingi yake imara iliyojiwekea.
Dk. Kikwete ameitoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo ya awali muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano huo wa NEC mbele ya waandishi wa Habari ambapo ameeleza kuwa, licha ya kuwa na maneno mbalimbali ya mitaani juu ya kukabidhi nafasi hiyo ya Uenyekiti kwa Rais Magufuli, aliwataka wana-CCM kuyapuuza maneno hayo kwani ni ya uongo na wala wasijisumbue nayo.
“Kuna watu wana mitambo yao ya vichochoroni ya kuzalisha bidhaa za uongo uongo tu. Tusiwape nafasi CCM imara na itaendelea kuwa imara Zaidi.
KUna watu walisema CCM itamfia, CCM itakufa, Kama haikufa sasa basi tena ndio haing’oki ng’o” alieleza Dk. Kikwete.
Katika Mkutano huo, ni wajumbe pekee wa NEC ndio wenye dhamana ya mkutano huo huku tukio kamili la kihistoria la makabidhiano ya kijiti cha Uenyekiti likitarajiwa kufanyika hapo kesho siku ya Jumamosi Julai 23.2016.
Waziri Mkuu Kasim Majaliwa akisalimiana na wajumbe wa NEC wakati akiwasili kwenye ukumbi wa Mkutano huo.
Baadhi ya sehemu ya Wajumbe wa NEC
Mbunge wa Nzega Vijijini na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na baadhi ya wajumbe wenzake wa NEC
Meza kuu ikiwasili ukumbini
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete (katikati) akiongoza kikao hicho cha NEC. Wa kwanza kushoto ni Rais Magufuli, akifuatiwa na Dk. Shein. Na upande wa kulia ni Katibu Mkuu wa Chama hicho, Mzee Kinana akifuatiwa na Mzee Mangula. (Picha zote na Andrew Chale, Dodoma.
Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu
akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call
Karibuni sana
LINK CLASSIC
LIKE PAGE ZETU
"KWA
HABARI ZAIDI "
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: