sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » SERIKALI YATAKA MAJIBU YA UGONJWA WA AJABU DODOMA

Serikali imeiagiza ofisi ya mkemia mkuu kutoa haraka majibu ya sampuli za vipimo vilivyochukuliwa kwa majeruhi wa ugonjwa wa ajabu uliozuka mkoani Dodoma na kusababisha vifo vya watu saba huku wengine 21 wakilazwa kwani kuchelea kutoa majibu hayo kunasababisha hofu kuzidi kutanda sambamba na kuzua mihemuko kwa wakazi wa maeneo yaliyokubwa na ugonjwa huo.

Waziri wa afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Mhe Ummy Mwalimu anatoa agizo hilo alipotembelea kijiji cha Mwakisabe kilichopo wilayani Chemba kinachodaiwa kuwa kiini cha kuibuka ugonjwa huo wa ajabu ambapo anasema kuchelewesha majibu ya vipimo vya sampuli kunaibua hisia tofauti kwa wakazi wa maeneo hayo ambapo sasa unahusishwa na imani potofu hali inayoweza kuhatarisha amani.

 Katika ziara hiyo waziri Mwalimu anakutana na baadhi ya watu  waliokula nyama ya Ng’ombe anayedaiwa anayesemekana ndio chanzo cha ugonjwa huo na hapa anatoa ushuhuda huku wakiwa na afya tele.

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Chemba Mhe Juma Nkamia anashangazwa na tukio hilo ambalo linazidi kuleta sintofahamu kwa wakazi wa wilaya za Kondoa na Chemba huku mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk James Charles anakanusha ugonjwa huo kuhusishwa na nyama kwani baadhi ya watu wamegundulika baadhi yao kutokula nyama hiyo.

KWA HABARI ZAIDI

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply