sponsor

Slider

T - SHIRT PRINTING


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » NDUGU WAWILI WA KIUME WAUAWA NA KUCHOMWA MOTO.

UNGANA NA 
LINK CLASSIC
KILA SIKU KWA HABARI MPYA

NDUGU wawili wa kiume waliuawa Alhamisi usiku na wanakijiji na kisha miili yao kuchomwa katika Kaunti ya Murang’a baada ya kuhusishwa na uhalifu.
Wenyeji wa kijiji hicho cha Njora kilichoko katika Kaunti ndogo ya Kigumo walisema kuwa wawili hao walikuwa washukiwa wa wizi na ambao walikuwa wakisakwa vikali kwa miezi minne iliyopita.
Bw Christopher Nuthu, 31 na kakake mdogo aliyetambuliwa kama Bw Peter Kamande mwenye umri wa miaka 29 walifurushwa kutoka nyumbani kwao mwendo wa saa tisa za usiku na kisha wakashambuliwa kwa vifaa butu hadi wakafariki.
Hatimaye, miili yao ilibururwa hadi barabarani na kuashwa moto.
Mabaki ya miili yao ilipatikana na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Njora ambapo ilikuwa imechomewa katika kiingilio cha shule hiyo.

Kwa mujibu wa Mkuu wa kamanda wa polisi wa Murang’a Bi Naomi Ichami, wanakijiji waliokuwa wamejihami walivamia wawili hao na baada ya
kuwafunga miguu na mikono wakitumia kamba, wakawaua.
“Baadaye walivuta miili hiyo hadi barabarani na kisha kuiwasha moto katika kisa hicho cha utovu wa nidhamu kisheria ambapo walichukua
sheria mikononi mwao,” akasema.
Alisema kuwa wanakijiji walikuwa wakilalamika kuwa washukiwa hao wamekuwa wakiwahangaisha kwa kuwavamia na kisha kuwapora nyumbani na pia katika barabara za eneo hilo.
Ugumu wa kuwakamata
Alisema kuwa ripoti zimekuwa zikipigwa katika kituo cha polisi cha Muthithi na ambapo tayari mikakati ya kusaka washukiwa hao ilikuwa ikitekelezwa.

“Kuwakamata kulikuwa na ugumu kwa kuwa wawili hao walihamia jijini Nairobi lakini wamekuwa wakiingia katika kijiji hicho nyakati za usiku na kisha kutekeleza visa vya uhalifu. Asubuhi na mapema huwa wanarudi jijini Nairobi,” akasema.
"Lakini wanakijiji walipata habari kuwa wawili hao wameonekana wakiingia kijijini na kisha vijana wakajikusanya na kutekeleza msako huo ulioishia kuwa wa mauti dhidi yao," akaongeza.
Mabaki ya miili hiyo yalipelekwa hadi Mochari ya Murang’a huku wenyeji wakisisitiza kuwa mhalifu yeyote katika eneo hilo hana bahati asipobadili mienendo yake.

“Tunataka kusafisha mji wetu kutokana na wezi. Polisi wamelemewa lakini sisi tutawaonyesha namna wezi hushughulikiwa,” akasema mwenyeji
mmoja aliyedai kushiriki mchakato huo wa kumaliza uhalifu.

Asante sana kwa kutembelea Website hii Mungu akubariki sana
+255 (0) 652989873 – Whatsapp / Call

Karibuni sana
LINK CLASSIC

LIKE PAGE ZETU 



"KWA HABARI ZAIDI "

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply