HALI si hali ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), baada ya Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Mwesigwa Celestine, leo asubuhi kufunga safari kwenda kwa Wizara ya Habari, Tamaduni, Sanaa na Michezo, kujadili kuhusu deni la Sh. Bilioni 1.600, wanalodaiwa na Mamlaka ya Mapato nchini TRA.
Katikati ya wiki mabasi matano ya TFF, yalikamatwa na na Madalali wa Mahakama (Yono Auction Mark) na TFF, kutakiwa kulipa deni hilo lililo anza tangu mwaka 2010 mpaka 2015.
Akizungumza na mtandao, mmoja ya watendaji wa TFF, aliyekataa kutajwa jina lake alisema hali ni mbaya na Katibu ameenda Wizarani kuzungumza ili aone kitu gani kinaweza kufanyika.
Mtendaji huyo alisema, licha ya Rais wa sasa wa TFF, (Jamal Malinzi) kuwa na dhamana ya deni hilo, lakini ‘amepigishwa shoti’ na kiongozi aliyepita.
“Asubuhi hii Katibu alituambia hali ni mbaya na anaenda Wizarani kujua nini hatima ya TFF na mabasi ambayo yamechukuliwa.
“Si kitu kizuri ambacho kimo humu ndani (TFF), lakini jamaa (Malinzi) hiki si kimeo chake, lakini yeye ndio kiongozi anayeshikilia hivi sasa, hivyo ni lazima abebe huo msalaba. Maana katika deni hilo kuna majumuisho ya mchezo wa Tanzania na Brazil mwaka 2010, muda ambao Malinzi hakuwa madarakani, lakini ndio hivyo wacha tuone nini mwisho wake”alisema mtu huyo.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: