sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » MAMBO MATATU YA KUKUSAIDIA KUJUA BIASHARA UNAYOTAKIWA KUIFANYA.


Pengine umekuwa ukiwaza, ukifikiri ni kwa namna gani au ufanye biashara ipi itakayokusaidia kukuingizia pesa nyingi na za kutosha. Na wakati mwingine umekuwa ukisumbuka pia kutafuta ushauri ni biashara gani ya kufanya. Hayo naamini ndiyo yamekuwa mawazo yako kwa muda mrefu.


Ikiwa kweli hayo ndiyo yamekuwa mawazo uliyonayo kwa muda sasa, hilo lisikupe shida. Unao uwezo mkubwa wa kujua na kutambua aina gani ya biashara unayotakiwa kuifanya na ikakupa faida. Je, unajua ni mbinu gani utatumia kutambua aina ya biashara unayotakiwa kuifanya?



1. Biashara uliyoichagua inauwezo wa kutatua tatizo katika jamii?  
Hapa sio suala tu kufanya biashara, je jiulize biashara hiyo ina uwezo wa kutatua matatizo ya watu kwa sehemu kubwa? Kama jibu ni ndiyo basi unaweza ukaifanya biashara hiyo na ikakuletea mafanikio. Lakini kama utajikuta umechagua biashara ambayo haina uwezo wa kutatua matatizo ya watu, hiyo haikufai na utapoteza muda wako kuifanya.

2. Je, unaipenda kweli biashara hiyo?
Biashara unayokwenda kuifanya uwe na uhakika itakuchukulia muda wako mwingi sana. Kitu cha kujiuliza wewe binafsi je,ni kweli una mapenzi nayo? Unaipenda na upo tayari kutoa kila kitu ili kufanikiwa. Haijalishi biashara yako inatatua matatizo makubwa vipi kwenye jamii kama huna mapenzi nayo ya dhati ni wazi utaiua na hutafika popote.

3. Je, upo tayari kukabiliana na changamoto?
Acha kutegemea ukaingia kwenye biashara leo na ukapata faida ni kitu ambacho hakiwezekani. Kama ni hivyo na unaona una wazo zuri la biashara yako, jiulize je utakuwa tayari kukabiliana na changamoto zozote zile zitakazojitokeza? Kama unaona uwezo huo unao, basi hakuna pingamizi unaweza ukaanza biashara yako mara moja.

Kwa msingi huo kama unataka kuanzisha biashara unayoamini itakupa faida, hayo ndiyo mambo ya msingi sana kwako kuyazingatia.

Na kumbuka endelea kujifunza kila siku bila kuchoka.


LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii

Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

+255 (0) 652989873 whatsapp



TWITTER    

LINKEDIN     DRIBBBLE

Karibu sana


LINK CLASSIC

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply