Hatimaye Shirika la Posta Nchini kufikisha huduma za Posta Mlangoni, ili kuendana na kasi ya awamu ya tano katika kuchangia ongezeko la uchumi wa kati nchini ifikapo 2025.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Kaimu Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta nchini Fortunatus Kapinga, amesema kuwa huduma hii itawawezeha wateja wenye anuani sahihi za makazi kufikishiwa barua, vifurushi na vipeto kwa urahisi zaidi tofauti na zamani ambapo ilimlazimu mteja afike katika ofisi za Posta na ilichangia upotevu wa vitu hivyo.
Akizungumzia hatua zilizofikiwa na Serikali kuhusu huduma hiyo Kaimu Posta Masta Mkuu huyo ameeleza kuwa mpaka sasa wamezifikia kata 32 kwa mkoa wa Dar es Saalam, Arusha 8 huku Zanzibar zikifikiwa kata 6 mbili za Unguja na nne za Pemba.
Wakati huduma hiyo ikitarajiwa kuzinduliwa siku ya Jumanne Kaimu Mkuu Kapinga ameitaja baadhi ya mikoa ambayo itafuatia kwa kuwekewa huduma hii ni Mwanza, Tanga, Morogoro, Kagera, Mara, Mtwara, Lindi,Shinyanga, Pwani, Manyara, Simiyu na Geita, pamoja na Tanzania Visiwani Unguja na Pemba kwa awamu ya pili, huku awamu ya Tatu ikijumuisha mikoa ya Songwe, Kigoma, Singida, Rukwa, Ruvuma, Katavi na Njombe kwa mwaka 2017 – 2018
LINK CLASSIC: Asante sana kwa
kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia
endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya
Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea
website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: