sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » HIZI HAPA FAIDA 8 ZA KUJIAJILI.


1. Ni njia bora ya kukufikisha kwenye uhuru wa fedha.
Inawezekana ukawa umechoka na kazi unayoifanya na unaoina haifai kwa namna moja au nyingine. Lakini njia bora ya kuweza kuondokana na utumwa huo ambao unakukabili ni kuanzisha biashara yako mwenyewe ambayo utaisimamia mpaka ikuletee mafanikio unayoyahitaji.

2. Ni Njia bora ya kujifunza.
Hakuna njia bora ya kujifunza kuhusu kutunza na kumiliki pesa kama biashara. Hili ndilo eneo  ambalo utajifunza mengi kuhusu masoko, namna ya kukuza mtaji na jinsi ambavyo unaweza ukaufikia uhuru wa kipesa. Kwa hiyo kama una biashara yako inakusaidia kujifunza yote hayo hatua kwa hatua.

3. Ni njia bora yakujifunza kujitegemea.
Unapokuwa kwenye ajira kwa kawaida unakuwa unamtegemea mtu fulani ambaye ndiye akuamulie juu ya maisha yako. Lakini kwenye biashara mambo hayako hivyo. Wewe ndiye unakuwa mwamuzi mkubwa wa maisha yako. Na unakuwa unakikisha unafanya kila linalowezeka mpaka biashara yako ifanikiwe.

4. Inakuwa inakupa hamasa ya mafanikio zaidi.
Huo ndiyo ukweli unaotakiwa ujue kuwa, unapokuwa na biashara inakuwa inakupa hamasa ya kuweza kufanikiwa na kusonga mbele zaidi. Tofauti na ajira ni rahisi kusema kuwa ‘aaah kazi yenyewe siyo yangu kwanza’ kwa hiyo unakuwa unafanya kwa jinsi unavyojisikia. Lakini kwenye biashara mambo hayako hivyo ni lazima kujituma ili kufanikiwa.

5. Inakuongezea ujasiri.
Unapokuwa mfanyabishara ni hatua nzuri sana kwako ya kukupelekea kuwa na ujasiri wa hali ya juu. Hiyo yote ni kwa sababu unapofanikiwa katika biashara moja unakuwa ndani yako una hamasa kubwa ya kutaka kufanya biashara nyingine tena kwa mafanikio. Kwa hali hiyo unakuwa una maamuzi mengi ya kijasiri ambayo ni rahisi kukusaidia kukusonga mbele.

6. Ni njia rahisi ya kufuata mipango na malengo yako.
Mara unapoanzisha biashara yako unakuwa upo kwenye njia sahihi ya kufuata ndoto za maisha yako. Hii yote ni kwa sababu unakuwa unakifanya kile kitu ambacho unakipenda kwa dhati toka moyoni mwako. Wakati unapokuwa kwenye ajira unakuwa unafanya tu ilimradi mkono uende kinywani. Hiyo ndiyo faida kubwa mojawapo ya kuwa kwenye biashara.

7. Inakufanya unakuwa ni mtu wa vitendo.
Watu wengi mara nyingi ni waongeaji bila ya kuwa watu wa vitendo. Lakini kitendo cha kuwa na biashara yako mwenyewe inakupelekea unakuwa ni mtu wa vitendo. Utaelewa vizuri umuhimu wa kuchukua hatua katika biashara tofauti na ambavyo ungekuwa hufanyi biashara ingekupelekea wewe kuwa na maneno mengi bila utekelezaji.

8. Ni njia bora ya kufanya mambo mengine zaidi.
Unapokuwa kwenye biashara inakuwa ni njia bora ya kufanya mambo mengine bora zaidi. Kama ulikuwa una lengo moja na umelikamilisha inakuwa ni rahisi kuweza kulifatilia lengo lingine mpaka tena kulifanikisha. Na hiyo nguvu yote ya kufanya mambo mengine inakuja kutokana na ujasiri ambao tayari unakuwa umeshajijengea kwenye biashara yako.

LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

+255 (0) 652989873 whatsapp



TWITTER    

LINKEDIN     DRIBBBLE

Karibu sana

LINK CLASSIC

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply