Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Vingunguti, Dk Modest
Mwinuka anasema wanawake wengi wanaofika hospitalini hapo
wanadai kuwa mimba imetoka yenyewe wanaogopa kusema ukweli
kwa kuhofia kukosa huduma. Dk Mwinuka anasema moja wapo ya
madhara makubwa ambayo yanampata mwanamke anayetoa mimba
vichochoroni ni kutoka kwa damu nyingi na kupasuka kwa kizazi.
“Madhara ya baadaye ni kupata maambukizi katika viungo vya uzazi,
kuharibikiwa mimba kila wakati kutokana na shingo ya kizazi kulegea pamoja na
kupata msongo wa mawazo,” Anasema kuwa madhara mengi ni kupata shida wakati wa
kuzaa kwa sababu shingo ya kizazi inakuwa imepata majeraha, kupata ugonjwa wa
Anemia kutokana na kutoka damu nyingi na pamoja na kupata shida ya kushindwa
kupata mimba kutokana na maambukizi katika viungo vya uzazi. “
Vilevile kuna madhara mengine ambayo ni mwanamke kupata ugumba,
mimba kutunga nje ya kizazi, kuzaa watoto wasio kuwa na akili nzuri, kupata
kansa ya mlango wa kizazi na kuathirika kisaikolojia,” anaongeza.
Muuguzi wa Chama cha Wauguzi nchini (Prinmat), Joseph Siga anasema
mfuko wa uzazi una utando maalumu ambao hufanya mimba iliyotungwa kwenye mirija
iitwayo fallopian kuwezesha yai kushuka hadi kwenye mifuko ya uzazi, Lakini
utoaji wa mimba huambatana na magonjwa ya mirija hiyo na kupoteza utando huo na
kusababisha mimba kukulia nje ya kizazi na matibabu ya tatizo hilo ni kukata
mrija husika husababisha kuongeza hatari ya ugumba.
“Wanawake wanaotoa mimba wana hatari kubwa
ya kupata kansa ya mlango wa uzazi kuliko wengine ambao hawajatoa mimba na hii
ni kwa sababu ya kusumbuliwa kwa mlango huo kwa dawa za kutoa mimba, vifaa vya
kutoa mimba na mabadiliko ya ghafla ya homoni za uzazi,”
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: