SAKATA la kukamatwa kwa tumbili waliokuwa mbioni kusafirishwa nje ya nchi, limechukua sura mpya baada ya idadi ya waliokamatwa mpaka sasa kufikia watu saba wakiwemo maofisa wanne wa serikali.
Miongoni mwa waliokamatwa ni Ofisa Mfawidhi Kanda ya Kaskazini anayehusika na Matumizi Endelevu ya Wanyamapori nchini Nyangabo Musika, Idd Misanya anayedaiwa kuwauzia wanyama hao.
Akizungumza , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mtafungwa aliwataja watu hao kuwa ni Juma Eliasa ambaye ni Mkurugenzi wa Manyara Bird wakiunganishwa na raia wa Uholanzi waliokamatwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA, Arten Vardanian (52) na Edward Vardanian (46).
“Tumewakamata watu hawa na bado tunaendelea na mahojiano zaidi, uchunguzi utakapokamilika tutawafikisha mahakamani,” alisema Kamanda Mtafungwa.
Wakati kamatakamata hiyo ikiendelea, wafanyabiashara wanaohusika na uwindaji wa wanyama hao wanalalamikia kitendo cha kukamatwa kwa wageni hao kuwa kitaathiri biashara yao hiyo.
LINK
CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja
ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL
zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia
waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp
+255 652 989 873
Karibu
sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: