
SERIKALI imetoa tamko kuwa kwa sasa haina mpango wa kuteketeza meno ya tembo yaliyohifadhiwa ambayo yametokana na vitendo vya ujangili na vifo asilia vya tembo.
Tamko hilo limetolewa hivi karibuni na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe alipokuwa anazungumza na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress.
Balozi huyo alimtembelea waziri Maghembe ofisini kwake kujadili maendeleo ya Sekta ya Maliasili nchini.
Akiwa hapo, alipendekeza Tanzania ichome sehemu meno ya tembo yaliyohifadhiwa ili kutoa ujumbe mzito duniani juu ya dhamira ya Serikali kukomesha biashara hiyo haramu.
Hata hivyo, katika majibu yake, Profesa Maghembe alisema; “Naomba niweke wazi kuwa kwa sasa hatupo tayari kuteketeza meno haya. Tunaweza kuyatumia kwenye tafiti za kisayansi au vielelezo kwa ajili ya kesi za ujangili ambazo zipo mahakamani na nyingine ambazo bado zinafanyiwa uchunguzi.”
Hatua hiyo imekuja huku nchi jirani za Kenya na Malawi zimeteketeza meno yake ya tembo yaliyohifadhiwa ikielezwa kufanya hivyo ni njia mojawapo ya kuishawishi dunia juu ya umuhimu wa kukomesha biashara haramu ya meno ya tembo. Nchi nyingine zilizofanya hivyo ni Chad, Ubelgiji, Ufaransa, China, India, Marekani na Ureno.
LINK
CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja
ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL
zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau
kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA


 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments: