Hali hiyo imemfanya mkuu wa wilaya hiyo Betty Mkwasa kuwa mbogo kwa watendaji wa vijiji na kata na kutoa siku saba watoto hao kuanza masomo mara moja sambamba na kuwafikisha wazazi wao mahakamani.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero Betty Mkwas atoa wiki moja kwa watendaji wa serikali za vijiji na kata vilivyopo wilayani humo kuwafikisha mahakamani wazazi na walezi walioshindwa kuwapeleka watoto waliochanguliwa kidato cha kwanza katika shule za sekondari na watoro sugu.
Mkuu huyo wa wilayao ameonekana kutoridhishwa na idadi hiyo ya wanafunzi kushindwa kuanza masomo wakati serikali imetoa elimu bure.
Kwa upande wao walimu na watendaji wamekiri kuwepo kwa tatizo hilo ambapo wameahidi kufuatilia watoto wote ambao hawajaripoti shuleni huku mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Wami Lupyana Kissya akieleza changamoto ya ukosefu wa walimu wa sayansi katika shule mbalimbali za sekondari ikiwemo shule yake.
Aidha Mkwasa akiwa katika ziara ya kikazi ya kutembelea shule za msingi na sekondari za wilaya hiyo ameendelea kutokuwa mpole baada ya kukuta baadhi ya vyumba vya madarasa kujengwa chini ya kiwango na kubomoka na kumuagiza mkurugenzi kumtafuta mkandarasi aliye husika na ujenzi wa darasa hilo na kulirudia kwa gharama zake mwenyewe na lianze kutumika maramoja.
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: