Wito huo umetolewa mkoani Mtwara na mkuu wa wilaya ya Mtwara, Fatma Ally, wakati wa ufunguzi wa warsha kwa wanafunzi wa sekondari na wadau wengine wa huduma zinazodhibitiwa, iliyoandaliwa na Jukwaa la watumiaji Tanzania (TCF), ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya haki za mtumiaji itakayofanyika kitaifa Machi 15 mwaka huu mkoani Mtwara.
Amesema kutokana na maeneo mengi ya vijijini kuwa na miundombinu migumu kwa kuweza kufikiwa na vyombo vya habari ambavyo vinatumika kutoa elimu hiyo, wananchi wengi wanakosa kupata elimu na itawafanya waendelee kutumia na kununua simu hizo ambazo ni bandia.
Kwa upande wake, katibu mtendaji wa baraza la ushauri kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mhandisi Goodluck Mmari, amesema maadhimisho hayo mwaka huu yanafanyika mkoani Mtwara kwa kuzingatia sababu mbalimbali ikiwamo kuwapo kwa fursa nyingi za kiuchumi zinazotokana na uwepo wa rasilimali za Mafuta na Gesi asilia.
LINK CLASSIC: Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu
mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna
vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa
na marafiki zako kutembelea website hii
pia waweza tupia namba yako
ukawa unapata habari kupitia simu yako bureeeeeeee...ila simu iwe smartphone
Pia waweza kuwasilina nasi
au kutufollow hapa chini
Whatsapp / Call - 0652 989 873
Karibu sana
LINK CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: