sponsor

Slider

EMBROIDERY, DTF, & SCREEN PRINTING - T-shirt, Overall, Shirt , Pylon, Kofia Nk..


LARGER FORMATING

STICKERS BRANDING | LARGE FORMATING


MIFUKO PRINTING

SMALL FORMATING

WEDDING | KITCHEN PART | SEND OFF | INVITATION CARDS

POSTERS | CARTOON | PHOTO PRINTING

» » » MBOWE AWAJIBU WALIOSEMA LOWASSA ALITOA FEDHA KUJIUNGA CHADEMA

MBOWE Mwanza 12/03/2016
MBOWE Mwanza 12/03/2016

Mwenyekiti wa Chadema-Taifa Freeman Mbowe  amesema, Edward Lowassa, aliyekuwa mgombea wa chama hicho kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana na kuungwa mkono na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hakutoa hata senti moja alipojiunga na chama hicho.

Mbowe amezungumza hayo kwenye Mkutano wa Baraza Kuu la Chadema leo Jijini Mwanza.

Amesema kuwa, pamoja na kuwepo kwa kauli nyingi kwamba, Lowassa alimwaga pesa kabla ya kujiunga na chama hicho, ukweli unabaki kuwa hakutoa pesa yoyote kama ilivyokuwa ikidaiwa.LOWASSA

 LOWASSA

“Watoto wangu walikuwa wanakula sana maharage, sasa siku moja wakala nyama, jirani akasema umeona Lowassa kaja Chadema,”amesema Mbowe.

Akizungumzia migogoro ya kichama iliyokuwa imejitokeza kwenye uchaguzi uliopita Oktoba 25 mwaka huu Mbowe amesema, kuna kila sababu kushughulikia migogoro hiyo kwa haraka.

“Migogoro mingi ndani ya Chadema imepelekea kuanguka kwa chama, hivyo itashugulikiwa kwa haraka,” amesema na kuongeza;Uchaguzi mkuu wa chama ni Oktoba 2018.”

Amewaeleza wajumbe wa mkutano huo kwamba, harakati za kisiasa hasa kukikuza chama ni gharama kubwa, jambo ambalo chama kinajitahidi kukabiliana nalo.

Amesema kwamba, pamoja na mambo yote ndani ya chama hicho lakini suala la rushwa haliwezi kuvumiliwa hata mara moja.

Akifafanua kauli hiyo amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeishi kwa kulea rushwa na kwamba, hali hiyo ndio imekifikisha hapo kilipo sasa.

Amesema, hali hiyo inaelekea kuingia Chadema jambo ambalo linaweza kusababisha kupasuka kwa chama hicho endapo halitashughulikiwa.

“Jambo ambalo hatutalivumilia ndani ya Chadema ni swala la rushwa kwani rushwa inagawa taifa, sasa swala la rushwa lililelewa na CCM na sasa inataka kuingia Chadema,” alisema.

“Kuna majimbo kama Iringa, Rukwa, Arusha Chadema waliachiwa kwa asilimia mia moja na Ukawa lakini kwanini wameshindwa kuchukua ushindi wa kutosha katika majimbo hayo?” alihoji.


LINK CLASSIC:  Asante sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako kutembelea website hii

pia waweza tupia namba yako ukawa unapata habari kupitia simu yako bureeeeeeee...ila simu iwe smartphone  

Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini

Whatsapp / Call - 0652 989 873

INSTAGRAM   FACEBOOK    GOOGLE+    PINTEREST   TWITTER       

LINKEDIN     DRIBBBLE   YOUTUBE

Karibu sana



LINK CLASSIC

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI

CODE HAPA

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Leave a Reply