Kesi namba 3/2015 ya kupinga matokeo ya uchaguzi ya mbunge wa jimbo la kinondoni Maulidi Mtulia (CUF) iliyofunguliwa na aliyekuwa mbgunge wa jimbo hilo Iddi Azan (CCM) imeshindwa kutolewa maamuzi hii leo kama ilivyokuwa imepangwa na mahakama kuu ya Tanzania.
Juma Nassoro ambaye ni wakili wa mshitakiwa Maulidi Mtulia ambaye ni mbunge wa kinondoni ameiambia www.mtembezi.com kuwa baada ya kesi hiyo kusikilizwa na Jaji Lugano Mwandambo kwa njia ya maandishi ilipangwa kutolewa maamuzi leo, ila kwa bahati mbaya Jaji huyo hakuweza kufika mahakamani kulingana na kupangiwa kushughulikia kesi zingine za uchaguzi mkoani Kilimanjaro, ambapo alimuomba Jaji Mfawidhi kumpanga jaji mwingine atakaye andika hukumu ya kesi hiyo, na hivyo wameambiwa kurudi tena kesho mahakamani kwa ajili ya kupangiwa tarehe nyingine.
Kwa upande wa mbunge Mtulia anayekabiliwa na kesi hiyo ameeleza kusikitishwa na kilichotokea kwa kile alicho dai kuwa kesi hiyo haina madai ya msingi na hivyo mahakama ilistahili kuitupilia mbali badala ya kuendelea kuipiga kalenda.
LINK CLASSIC: Asante
sana kwa kutembelea Website hii coz ni moja ya Support kwetu mungu akubariki
sana pia endelea kusoma na kufungua LEBAL zingine kwani kuna vingi vizuri zaidi
ndani ya Website hii bila kusahau kuwashirikisha ndugu jamaa na marafiki zako
kutembelea website hii
Pia waweza kuwasilina nasi au kutufollow hapa chini
Whatsapp +255 652 989 873
Karibu sana
LINK
CLASSIC
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: