1. Jitahidi kufanya KAZI au kusomea kitu ukipendacho hii itakusababisha uweze kuwa na juhudi katika kukifanya maana ni kitu ukipendacho.
2. Ishi kutokana na kipato chako, usipende kuiga maisha ya watu wengine wakati uwezo wenu unatofautiana.
3. Kabla hujafika miaka 30 tengeneza mwili uutakao na uweze kuutunza usizidi wala kupungua hapo utakapo.
4. Katika mapato unayopata jitahidi angalau uweke asilimia 30 akiba ya mapato, usisubiri upate fedha nyingi sana, kidogo kidogo utajikuta na akiba nyingi sana.
5. Ni vyema kujipanga kabla hujaingia katika ndoa maana ndoa inahitaji ujiandae kisaikolojia na umri mkubwa sio kigezo bal kigezo ni utayari.
6. Chagua marafiki wenye mawazo mazuri katika maisha yako na sio bora marafiki maana marafiki wana nafasi kubwa maishani mwako, ukichagua vibaya utajuta baadaye.
7. Acha starehe zisizo na muhimu sana.
8. Kama ni mfanyakazi jitahidi kuwa na biashara nyingine pembeni ya kukuingizia kipato ili usitegemee sana mshahara.
9. Zaa watoto kutokana na uwezo wako wa kuwalea ili watoto wawe na maisha mazuri.
10. Unapotaka kuingia katika ndoa, ingia na mtu unayempenda na ujiandae kisaikolojia kuwa katika ndoa kuna mambo mazuri na mabaya hivyo uwe mvumilivu.
SHARE na kwa wengine tukumbushane.
KWA HABARI ZAIDI
BOFYA HAPA KU DOWNLOAD APPS YA LINK CLASSIC USOME HABARI KIRAHISI NA HARAKA ZAIDI
CODE HAPA
No comments: